Nahodha wa Tanzania Mbwana Samatta amejiunga na club ya Fenerbahce ya Uturuki akitokea Aston Villa ya England, inaripotiwa Fenerbahce wamemsajili kwa mkopo wa msimu mzima 2020/21 lakini Sky Sports wao wametangaza kuwa Samatta amesajiliwa jumla kwenda Fenerhbace kwa mkataba wa miaka minne.
Unajua Samatta hajakaa sana Aston Villa na wengi kutaka kujua kwa nini anaondoka mapema Aston Villa akiwa amekaa kwa miezi tisa tu licha ya kusaini mkataba wa miaka minne na nusu mwezi January 2020 akitokea KRC Genk ya Ubelgiji.
AyoTV imeongea na Mtanzania Salim Kikeke ambaye anaishi na kufanya kazi London England katika shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), kwa mtazamo wake nini kimemkwamisha Samatta? mashabiki wa Aston Villa wamelipokeaje, Samatta anaondoka Aston Villa akiwa kaichezea michezo 16 na kuifungia magoli mawili pekee.