Fahyvanny "Rayvanny Kwangu Amefika Kigoma Mwisho wa Reli"



MZAZI mwenza wa msanii wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny, mwanadada Fahima Msenga ‘Fahyvanny’ amekiri kuwa hatoweza kuachwa na mpenzi wake.


Mwanadada huyo ambaye pia ni maarufu kama Fahyma, amesema amewaponda wale wanaodai kuwa ameachwa na mumewe huyo na kudai kuwa, kwa Rayvanny ndiyo kashafika.


Katika kuthibitisha hilo, aliposti picha katika  mtandao wake wa Instagram, ambapo mashabiki walimtaka kupunguza stesi kwa kuwa mume harudishwi kwa kufanya hivyo.


Hata hivyo, Fayvanny naye alijibu na kuwaambia “Kiufupi kwangu ndiyo kashafika na mimi ndiyo mwanamke wa maisha yake, hivyo hawezi kuniacha na desturi ya Watanga hatufunzwi”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad