Familia ya Khashoggi yaridhika na hukumu kwa wauaji wake




Familia ya Jamal Khashoggi, mwandishi wa habari wa gazeti la Washington Post aliyeuawa katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia nchini Uturuki, imesema hukumu iliyotolewa kwa watu waliomuuwa ni ya haki, na inaweza kuzuia uhalifu mwingine kama huo.

 Hayo yameripotiwa katika gazeti la Asharq Al awasat linalomilikiwa na serikali ya Saudi Arabia. Hapo jana mahakama ya Saudi Arabia iliwahukumu watu wanane kifungo cha miaka kati ya saba na 20, kwa hatia ya mauaji ya Khashoggi yaliyofanyika mwaka 2018. 


Hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya uhalifu mjini Riyadh ilitangazwa na televisheni ya taifa, lakini majina ya watu hao waliotiwa hatiani hayakufichuliwa. 


Wakati kesi hiyo ikihitimishwa nchini Saudi Arabia, bado kuna kiwingu kuhusiana na nafasi ya kimataifa ya mwanamfalme mrithi wa Ufalme Mohammed bin Salman, ambaye washirika wake wamewekewa vikwazo na Marekani na Uingereza kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji hayo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad