Mashabiki wa Fid Q na Joh Makini sasa jiandaeni kugonga glasi pamoja. Kwa miaka mingi sasa kwenye muziki wetu mashabiki wamekuwa wakisubiri Kolabo kati ya vinara hawa wa Hip Hop nchini.
Kwenye tafsiri ya vichwa vya waswahili ni kwamba wawili hawa hawapikiki chungu kimoja ndio maana Kolabo hiyo imechelewa kufanyika, tofauti na zile za kila siku kati ya Fid Q na Lord Eyez wa WEUSI.
Jana kupitia #E20Countdown na @bdozen, Fid Q ametupa habari njema kuhusu kushirikiana na Joh Makini kwenye wimbo mmoja hivi karibuni, Ngosha awali alikuwa akihojiwa na kusema Kolabo hiyo inashindikana kwasababu haoni muunganiko kati yao (Chemistry) lakini katika kipindi cha hivi karibuni ameanza kuona hilo na Kolabo hiyo itafanyika.