Producer wa wimbo Kanyor Aleng wa @rosa_ree , @ibrah_jacko amelipwa pesa zake na @harmonize_tz baada ya Rais huyo wa label ya @kondegang kutumia beat ya wimbo huo kwenye wimbo wake, Amen bila makubaliano.
Mapema wiki hii mwanasheria wa COSOTA, Lupakisyo Mwambinga aliiambia Bongo5TV kwamba moja ya kesi walizozisimamia na zimeisha salama ni ile ya producer Ibrah kudai beat yake ambayo aliitengeneza kwaajili ya wimbo Kanyor Aleng wa @rosa_ree kutumiwa na @harmonize_tz bila makubaliano.
Bongo5TV baada ya kumtafuta producer huyo alikiri kupipwa na Harmonize na kueleza jinsi ilivyokuwa.
Kwa upande wa manasheria wa COSOTA amewataka wasanii kuacha kufanya kazi na maproducer bila mikataba ili kuepuka migogoro.