Heche amkabidhi Lissu kero za mji wa Sirari



Mgombea ubunge jimbo la Tarime Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA,John Heche amemkabidhi Kero za mji wa Sirari mgombea urais,Tundu Lissu ili kuzishugulikia endapo atachaguliwa na wapiga kura.


Heche alisema kuwa wakazi wa mji wa sirari wanakabiliwa na changamoto ya kubambikiwa kesi za kuwa wao sio raia wa Tanzania pindi wanapojitokeza kugombea hususani kupitia tiketi ya CHADEMA.


Nikuombe Mgombea wetu wa nafasi ya Rais endapo wapiga kura watakuamini na  kukuchagua  uhakikishe kuwa unamaliza kero iliyopo ya watu wa Sirari ya kubambikiwa kesi kuwa wao sio watanzania hususani wale wanaokuwa wanajitokeza kugombea nafasi za uongozi kupitia CHADEMA licha ya kuwa watu wa sirari wanaishi mpakani mwa Tanzania na Kenya”alisema Heche.


Heche aliongeza kuwa mahitaji  makubwa ya wakazi wa mpakani wanategemea bidhaa kutoka nchi jirani ya Kenya kwa sababu gharama ni nafuu ya kununulia ikilinganishwa na bidhaa za Tanzania.


Heche alitolea mfano ya kero hiyo kuwa  ukikamatwa  na mfuko mmoja wa sementi  unasiziwa chombo kilichobeba pamoja na bidhaa sasa ukifanikiwa na kupewa  ridhaa ya wananchi  kuwa rais na uhakikishe sheria hiyo inaondolewa.


Mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumchagua,Tundu Lissu na kuwa Rais pamoja Heche kuwa Mbunge pamoja na madiwani wote wanaotokana na CHADEMA ili kwenda kushugulikia tatizo la maji ambapo mchakato umeisha anza wa kutoa maji ziwa Victoria.


Akitolea mfano mgombea wa tiketi ya CHADEMA nafasi ya udiwani kata ya Sirari,Denson John Makanya,Heche alisema mgombea huyo amewekewa pingamizi kuwa ni Mkenya jambo ambalo halikubaliki.


Kwa upande wake mgombea urais,Tundu Lissu aliwaomba wananchi kumchagua pamoja na wagombea wote wanaotokana na CHADEMA ili kumaliza kero zinazowakabili watanzania pamoja na watu wa sirari.


Lissu aliongeza kuwa kukaa mipakani ni frusa na wala sio laana mtu kuzaliwa mpakani mwa nchi jirani  bali ni mipango ya Mwenyezi Mungu na inafunguia baadhi ya frusa za kiuchumi na kibiashara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad