Hoja ya CCM kujaza watu kwa kutumia wasanii



Kumekuwa na mjadala kidogo kwa baadhi ya watu wakihoji kuhusu namna mgombea wa Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli anavyoendelea kujaza mamia kwa mamia ya watu kwenye mikutano yake tena mpaka kwenye maeneo anayosimama tu kwa muda kusalimia. Kila mmoja akizungumza yake kuhusu nyomi hiyo.

Kwa bahati mbaya sana wako wanaodai nyomi na mafuriko hayo yanasababishwa ati na watu kufuata kuangalia wasanii tu wanaokuwa kwenye mikutano ya mgombea huyo wa Urais. Hawajiulizi mbona hata kwenye maeneo anayosimama tu kwa dakika kadhaa kusalimia watu hufurika isivyo kawaida. Mfano Jana pale Nyakato, Mabatini na Igoma watu walijaa mpaka ikafikia kiwango cha barabara kuziba kwa watu kujaa kwenye barabara. Hawajiulizi hapo alikuwa na wasanii gani?

Kwa CCM uchaguzi huu ni sherehe ya kusherekea mapinduzi makubwa yaliyofanyika kwa miaka mitano tu na kuelezana tulikotoka, tulipo na tunakoelekea. Kwa hiyo huu ni uchaguzi wa kuambiana mafanikio makubwa tuliyoyapata na sasa kukumbushana tu na Watanzania wenzetu kwenda kumaliza kazi Oktoba 28.

Kwahiyo tunakutana na wananchi wenzetu kusherekea ushindi mkubwa wa wafanyabiashara wadogowadogo baada ya mateso makubwa waliyoyapata huko nyuma kwa kuonewa, kutozwa matozo kila siku na kufukuzwa kila mahali kufanya biashara zao. Leo hakuna mmachinga wala mfanyabiashara mdogo anayeonewa kwenye ardhi hii ya Tanzania. Kwanini tusisherehekee na Watanzania wenzetu?

Kwanini tusisherekee mzigo tuliowatua akinamama waliokuwa wanapata shida mahospitalini, kutukanwa na watoa huduma, shida ya huduma za uzazi na dawa. Leo hakuna mama anayeona na kupata shida nchi hii. Kwanini tusisherekee.

Uchaguzi huu kwa CCM ni kukutana na wananchi wake kusherekea kwa pamoja ushindi huu mkubwa kwenye kila eneo la maisha ya Mtanzania kuanzia kwenye huduma za afya, miundombinu, ulinzi wa rasilimali zetu na ukuaji uchumi wetu mkubwa wa miaka mitano tu uliopatikana. Watanzania wameona na ndio mana wanakuja tusherekee pamoja na baadae wakafanye maamuzi siku ya Oktoba 28 ili kwa pamoja tukamalizie mkia uliobaki baada ya ng'ombe nzima kumla.

Bwanku M Bwanku
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad