Bill Edgar anawawakilisha waliofariki. Anahudhuria mazishi na kuzungumza kwa niaba ya marehemu kuwasilisha ujumbe ambao hakuweza kuwasilisha alipokuwa hai. Anasema kuwa ana visa vingi vya kusimulia
Pia analipwa hela nyingi kutokana na kazi hiyo.
Alianza vipi kazi hii?
Bill alikuwa anafanya kazi kama mpelelezi wa kibinafsi wa mtu mmoja raia wa Australia ambaye alikuwa anaugua maradhi ambayo hayana tiba, wazo hilo lilipomjia.
“Tulianza kuzungumzia kifo na maisha baada ya kifo na mambo mengine mengi. Mara akainiambia, Naomba unifanyia jambo fulani wakati wa mazishi yangu’. Nami nikapendekeza andike wasifu wake mwenyewe.”
Mwanamke akifarijiwa wakati wa mazishi ya mpendwa wake
Familia yako itafikiria nini ukimtumia mtu kuingilia kati mazishi yako mwenyewe?
Lakini mtu huyo alisema familia yake na marafiki hawatafurahia ujumbe huo, pengine huenda wasiusome ama kucheza kanda ya sauti itakayokuwa imerekodiwa.
“Nikapendekeza kuingilia kati ratiba ya mazishi kwa niaba yake. Na hivyo ndivyo nilivyoanza kazi hii.”
Analipwa pesa ngapi kufanya kazi hiyo?
Bill sasa anaingilia kati ratiba ya mazishi kuwasilisha ujumbe wa marehemu kwa walio hai. Yeye ni ‘mfichua siri za marehemu’, ambayo inamaanisha hivi kwa maneno yake mwenyewe, “Wakati ibada ya mazishi ikiendelea, Ghafla nasimama, nafungua bahasha na kuanza kusoma ujumbe nilioandikiwa na marehemu wakati alipokuwa hai.”
Kwa malipo ya karibu dola 7,000, Bill anaweza kuhudhuria mazishi kumwakilisha marehemu iwe ni kwa kusoma wasifu wake ama kufichua siri kwa niaba ya marehemu, wakati mwingine huenda akaangazia mambo ambayo ni ya kibinafsi sana na ambayo huenda yasiwafurahishe waombolezaji.
“Huenda ikawa ni tabia ya marehemu ambayo aliweka siri kwa uraibu wa ngono, kutumia vifaa vya kujichua, dawa za kulevya, pesa – ama kitu chochote.”
Ushawahi kujiuliza ni kitu gani mtu aliamua kuweka siri hadi akafariki bila kusema?
Ushawahi kujiuliza ni kitu gani mtu aliamua kuweka siri hadi akafariki bila kusema?
Visa ambavyo havijawahi kuangaziwa
Kazi anayoikumbuka sana ni ile alioyoombwa na marehemu avuruge hotuba itakayotolewa na rafiki yake wa karibu.
“Ilinibidi nimwambie nyamaza na ukae chini usikilize ujumbe niliyoandikiwa na marehemu ni uwasilishe kwako… na hapo nikaanza kusoma. Ujumbe ulikuwa unasema rafiki wa marehemu alijaribu kumtongoza mke wake wakati alipokuwa hali mahututi.”
Baada ya Bill kufanya hivyo, yule bwana alitoroka kupitia ”mlango wa nyuma” na kwenda zake. Watu wengine kadhaa waliombwa kuondoka katika hafla hiyo ya mazishi – kwa niaba ya marehemu na baada ya hapo Bill anasema, “mazishi yaliendelea vyema”.
Staged picture of a funeral procession with a group of mourners standing in the rain
Mazishi ni ya nani hasa: kati ya aliye hai na aliyefariki?
Kutokana na sababu ambazo zinaeleweka, Bill hapokei mrejesho wowote kutokana na kazi yake kama vile tathmini au malalamishi kutoka kwa wateja wake wa zamani. Lakini cha kushangaza hajawahi kufukuzwa mazishini na walio hai.
“Naelezea waombolezaji mambo ya kushangaza kumhusu marehemu, lakini ni mazishi yao, kwa nini wasiagwe wanavytaka wao?”
Bill Edgar alizungumza na BBC katika kipindi cha Newsday. Unaweza kusikiliza mahojiano yake hapa.