Ijue Siri Ya Kuondokana Na Ukata wa Pesa na Umaskini

Siku ya leo katika pekua pekua zangu za kuongeza chakula cha ubongo nilikutana na kauli ambayo kiukweli ilifanya mishipa yangu ya ardenalini kuweza kushtuka kwa kasi kama vile nimeona kitu cha hatari sana.

Kauli hiyo ilikuwa na maneno mawili yenye kubeba ujumbe mzito ambao sina uhakika kama, ujumbe huo upo mzani ambao ataweza kupima kilo zake, hii ni  kutokana na uzito uliopo katika ulipo katika ujumbe huo,  labda ujumbe huo upimwe na kichwa cha mwanadamu mwenye mtazamo chanya ndio anaweza kuuelewa.

Ujumbe huo unasema “unachokiogopa ndicho kitakachokua” narudia kusema tena unachokiogopa ndicho kitakachokua. Kwa haraka haraka unaweza usielewe maana ya msemo huo ila pindi utulizapo fikra ya ujazo wa akili unaweza kuelewa.

Binafsi nilichokielewa katika kauli hii ni kwamba, moja kati changamoto kubwa ambayo huwazuia watu wake kutoweza kutimiza makusudio yao hapa dunia ni kitu ambacho tunachokiita ni woga.

Woga ndio ambao umekua tatizo sugu lilojengeka machoni mwa watu wengi hata kuwapelekea watu hao kuweza kufa maskini huku watu hao wana uwezo mkubwa wa kufanya mambo makubwa yenye kuleta mapinduzi ya kufikia kilele cha mafanikio yao.

Woga huu si mwingine ni ule woga wa kuthubutu kuweza kufanya mambo mbalimbali. Wapo watu ambao wanatamani kufanya biashara kubwa ila wakiwatazama watu ambao walifanya biashara hiyo na kuona ya kwamba walifeli basi nao hujikuta wanaogopa kufanya jambo hilo.

Achilia mbali biashara, wapo baadhi ya watu wanavipaji mbalimbali lakini watu hao wamekuwa ni waoga wa kuonesha vipaji hivyo machoni mwa watu wengine huku wakiamini ya kwamba watachekwa, watu wa aina hii mara nyingi hufa na ndoto zao.

Wapo baaadhi ya watu wanaogopa kujenga nyumba zao za kuishi huku wakisema, “kwa heshima niliyonayo nikijenga nyumba ya kawaida watu wengine wanatanishangaa” kwa kauli kama hizi basi hujikuta miaka inazidi kukatika bila watu hao kuweza kufanya kitu chochote cha maana.

Wapo baadhi ya wanafanzi wamekuwa wanaogopa kusoma masomo ya sayansi huku wakiamini masomo hayo ni magumu mwisho wa siku watu hao hujikuta wanafeli masomo hayo, kwa mtazamo wa aina hii ndipo ninapokubaliana na kauli ile ambayo nimesema hapo awali ya kwamba unachokiogopa ndicho kitakachokua.

Kabla sijamaliza kusema nawe siku ya leo nitakuwa ni mchoyo wa fadhira kama nitashindwa kutoa ufumbuzi wa tatizo hili, yawezekana ukawa na tatizo la aina hii ya kuogopa kufanya jambo fulani la maendeleo eti kwa sababu ya woga uliojengeke ndani mwako, unachotakiwa kukufanya ni kuhakakisha kila jambo ambalo unataka kulifanya, kabla hujaanza kulifanya jambo hilo hakikisha ya kwamba jambo hilo unalichunguza kwa makini  na sio kutanguliza woga mbele na ndiyo itakuwa siri ya kuondokana na ukata.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad