Iran yatoa hukumu ya kifo kwa mwanamieleka aliyehusishwa na mauaji



Iran imemhukumu kwa kumnyonga kijana mwanamieleka, Navid Afkari kutokana na kukutwa na hatia ya mauaji ya mfanyakazi wa umma katika kipindi cha maandamano ya kuipinga serikali ya taifa hilo ya Agosti 2018.

Mwendesha mashitaka wa jimbo Kazem Mousavi amenukuliwa katika tovuti ya televisheni ya umma akisema Afkari amenyongwa asubuhi ya leo katika gereza lililopo mji wa kusini wa Shiraz.

Kwa mujibu wa mahakama kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 alikutwa na hatia ya mauwaji kwa kumchoma na kitu chenye ncha kali Hossein Torkman, mfanyakazi wa kitengo cha maji, mkasa ambao unatajwa kutokea Agosti 2018.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter wakili wa Afkari, Hassan Younessi, amesema watu kadhaa mjini Shiraz wanapanga kwenda kukutana na ndugu ya mfanyakazi aliyeuwawa Jumapili kwa ajili ya kumuombea msamaha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad