Iran yautaka ulimwengu kuungana dhidi ya ''vitendo vya ovyo'' vya Marekani



Iran leo imetoa wito kwa ulimwengu mzima kuungana dhidi ya kile inachosema ni "vitendo vya ovyo'' vya Marekani baada ya nchi hiyo kutangaza kurejeshwa kwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya taifa hilo la Kiislamu. 

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran, Saeed Khatibzadeh, amewaambia wanahabari mjini Tehran kuwa wanatarajia jamii ya kimataifa kuungana dhidi ya vitendo hivyo vya serikali ya Marekani na kuzungumza kwa sauti moja. 


Wakati huo huo, wizara ya mambo ya nje ya Urusi leo imetuhumu tamko hilo la upande mmoja la Marekani kwamba vikwazo dhidi ya Iran vimerejeshwa tena na kusema hatua hiyo sio halali na haikubaliki. 


Katika taarifa yake, wizara hiyo imesema kuwa mikakati na vitendo vya Marekani visivyokuwa halali haviwezi kuwa na athari za kisheria za kimataifa kwa mataifa mengine. 


Hapo jana Marekani ilitangaza kuwa vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vimeanza tena kutekelezwa na kutishia kuwaadhibu wale watakaovikiuka. 


Hatua hii huenda ikaendeleza kutengwa kwa Marekani kilimwengu na pia kuzusha mivutano ya kimataifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad