Jafo atoa wito kwa wanafunzi waliokosa vigezo kidato cha tano kujiunga vyuo vya kati
0
September 02, 2020
Wanafunzi waliokosa nafasi za kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa kukosa tahasusi zinazokidhi vigezo wameshauriwa kuomba nafasi za masomo katika vyuo vinavyosimamiwa na NACTE ili kuweza kpata nafasi ya kuendelea na masomo katika vyuo hivyo.
Wito huo umetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Seikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo leo Jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu matokeo ya uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya pili .
“Wanafunzi waliochaguliwa wote wanatakiwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano awamu ya pili kuhakikisha wanafika shuleni kuanzia Septemba 6 hadi 20 mwaka huu ambapo mwanafunzi atakeyeshindwa atakuwa amepoteza nafasi yake”, amesisitiza Mhe. Jafo.
Aidha Mhe. Jafo amesema kuwa jumla ya wanafunzi 1,017sawa na asilmia 11.82 wamekosa tahasusi zinazokidhi vigezo na kwa sababu hiyo hawajachaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano katika awamu ya pili.
Mhe. Jafo amesema kuwa kati ya wanafunzi waliochanguliwa ambao ni asilimia 88.18 ya waliokosa nafasi awamu ya kwanza walikuwa wasichana 1,109 na wavulana ni 6,477.
Mhe. Jafo ameeleza kuwa kuwa wanafunzi 7,586 kati ya 8,603 walikosa nafasi awamu ya kwanza wamechaguliwa kijiunga na kidato cha tano katika awamu ya pili.
“Baada ya kukamilika kuchagua wanafuzi wa kujiunga kidato cha tano awamu ya kwaza, wanafunzi 8,603 wakiwamo wasichana 1,281 na wavulana 7,322 hawakupangiwa shule”,ameeleza Mhe. Jafo
Hata hivyo Mhe. Jafo amesema kuwa wanafunzi 355 ikiwa ni wavulana 254 na wasichana 101 wamebadilishwa kutoka vyuo mbalimbali na kujiunga na masomo ya kidato cha tano.
Katika hatua nyingine Mhe. Jafo amesema kati ya wanafunzi waliochaguliwa, wanafunzi 615 wamepangiwa tahasusi za sayansi na hisabati na wanafunzi 6,971 wamepangiwa tahasusi za masomo ya sanaa na biashara
Tags