Jamii ya Pwani na Utamaduni wa Sherehe za Kumtoa Binti Mwali.....


Katika baadhi ya Mikoa na Pwani ya Tanzania, wana utamaduni wa binti kupatiwa Mafunzo Maalumu ya Kimila au maarufu kama 'Kufundwa' na hujumuisha wasichana kuwekwa ndani kwa muda wa miezi kadhaa

Kwa binti ambaye hajapitia tukio hili huonekana kama atakuwa na hasara kubwa katika maisha yake ya ndoa ya baadaye kwani huonekana kama vile hajui mambo mengi ya kumridhisha mume kwa mujibu wa mila

Miongoni mwa Jamii inayotajwa kuendeleza mila hizi ni Wamakonde kutoka Kusini mwa Tanzania na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Pwani, ndani na hata nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam

Wazawa hawa wanamcheza binti kuanzia umri wa miaka 10 ambapo binti huelekezwa unyumba, namna ya kukaa na mume, nguo za kuvaa akiwa na mumewe, chakula cha kupika na kadhalika

Aidha, utamaduni huu umekuwa ukilaumiwa na baadhi ya watu kuwa ndio chanzo cha kusitisha masomo kwa wasichana wengi pamoja na mimba za utotoni kwani sherehe hizi zinafanyika wasichana wanapomaliza darasa la 7 au hata kabla hawajamaliza elimu hiyo

Ni tamaduni nyingine zipi zinazofanyika kwenye Jamii inayokuzunguka?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad