Mamiss hao kutoka kushoto, Genevieve Mpangala, Hapiness Magese, Jaquiline Mengi, Nancy Sumari na Queen Elizabeth Makune.
Miss Tanzania mwaka 2000 Jaqueline Mengi kwa kushirikiana na mamiss wenzake waliwahi kushika taji hilo wameanzisha mpango wa kuwahamasisha wasichana na wanawake kuchangisha fedha za kusaidia afya na elimu.
Akizungumza na wanahabari jijini Dar leo Jaqueline amesema mpango unaoitwa Beauty Legacy 2020 utazinduliwa Novemba 14 mwaka huu kwenye Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro Hotel) Jijini Dar es Salaam.
Hivyo ameyataka makampuni, watu binafsi na wengineo kujitokeza kufadhili shughuli hiyo ambayo itakwenda kuwasaidia watoto waliozaliwa kabla ya umri (njiti), kutoa miguu bandia kwa watu wanaishi na ulemavu, kufanya ukarabati wa wodi za wazazi na miradi mingine kama hiyo na kusaidia sekta ya elimu.
Katika mkutano huo na wanahabari baadhi ya warembo waliohudhuria mkutano huo ni pamoja na Miss Tanzania 2018, Queen Elizabeth Makune, Miss Tanzania 2010 Genevieve Mpangala, Miss Tanzania 2005 Nancy Sumari, Miss Tanzania 2001 na Hapiness Magese.
Jaqueline amesema mamiss waliowahi kutwaa taji hilo wanatarajiwa kuwepo kwenye uzinduzi huo wa Septemba 14 mwaka huu.