JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 09



JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa 09 kwa tuhuma za makosa mbalimbali yakiwemo Uporaji, Wizi na Uvunjaji. 

KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA WA MATUKIO YA WIZI WA PIKIPIKI NA UPORAJI.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wanne 1. BEATUS ANDREA [28] Mkazi wa Uyole, 2. JAMES MWAKABOKO [27] Mkazi wa Forest, 3. HILMAL HAULE [40] Mkazi wa Mbozi, Mkoa wa Songwe na 4. BAHATI GERSON [22] Mkazi wa Ubaruku kwa tuhuma za wizi na uporaji wa Pikipiki.

Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 16.09.2020 majira ya saa 11:44 asubuhi huko Mtaa wa Eso Jijini Mbeya, Kata ya Forest, Tarafa ya Iyunga na timu ya makachero wa Polisi wakiwa wanafuatilia watuhumiwa wa matukio ya uporaji na wizi wa Pikipiki. Watuhumiwa wamehojiwa na kukiri kuhusika na matukio ya wizi na uporaji wa Pikipiki ikiwemo Pikipiki MC.395 CPG aina ya TVS rangi ya bluu na kwamba tayari wameipeleka nchini Malawi kwa mtu aitwaye SELEMAN MLAWA PINDA. Upelelezi wa shauri hili unaendelea.



KUINGIA NDANI YA HIFADHI BILA KIBALI.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa watano 1. ABUBAKAR AMIR [32] Mkazi wa Wilaya ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga 2. FADHILI HAMIS @ KANDI [32] Mkazi wa Igomaa – Mufindi, 3. KADRI UHURU [31] Mkazi wa Igomaa – Mufindi, 4. MASHAURI MWILINGWA [40] Mkazi wa Igomaa – Mufindi na 5. ATHUMANI NADA [35] Mkazi wa Mianzini – Arusha kwa tuhuma za kuingia ndani ya hifadhi bila kibali.


Watuhumiwa walikamatwa mnamo tarehe 16.09.2020 majira ya saa 13:00 mchana huko ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, Kijiji cha Ngirayama, Kata ya Lugelele, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya.  Watuhumiwa waliingia ndani ya hifadhi ya Ruaha bila kibali na walikutwa na mchanga udhaniwao kuwa na madini aina ya dhahabu katika mifuko 06 ya sandarusi yenye uzito wa kilo 640. Upelelezi unaendelea.


AJALI YA MOTO.


Mnamo tarehe 17.09.2020 majira ya saa 11:00 asubuhi huko Mtaa wa Maendeleo, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya. Nyumba ya KENNEDY ERASTO [30], Mfanyabiashara ndogo ndogo na Mkazi wa “Airport” ya zamani yenye vyumba vinne[04] na sebule iliungua moto na kuteketeza mali zote zilizokuwa kwenye vyumba viwili na sebuleni zikiwemo samani. 


Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea. Thamani ya mali iliyoteketea na uharibifu bado kufahamika. Chanzo kinachunguzwa. Moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Jeshi la Polisi, TANESCO na Wananchi. Ufuatiliaji unaendelea.


 TAAFRIFA YA KIFO.


Mnamo tarehe 15.09.2020 majira ya saa 17:30 jioni huko Kitongoji cha Shoga, Kijiji na Kata ya Sangambi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, wachimbaji wadogo wa dhahabu wawili ambao ni SHABANI FUNGO [38] Mkazi wa Kyela na UWEZO MWANYOMBOLE @ ABASI [34] Mkazi  wa Kiwanja  -  Chunya walifariki dunia baada ya kifusi cha udongo kufunika shimo walilo kuwa ndani wakichimba madini ya dhahabu bila kuchukua tahadhari. Chanzo cha kifo ni kukosa hewa. Miili ya marehemu imefanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kuhifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Chunya kusubiri kukabidhiwa ndugu kwa mazishi.



UNYANG'ANYI WA KUTUMIA NGUVU.


Mnamo tarehe 18.09.2020 majira ya saa 01:50 usiku huko Mtaa wa Mwanyanje uliopo Kata ya Igawilo, Tarafa ya Iyunga, Jiji la Mbeya. BOAZ PAULO NYUDULA [45], Mfanyabiashara na Mkazi wa Mwanyanje alivamiwa na watu wapatao sita wasiofahamika wakiwa na marungu, nondo na fimbo na kuvunja milango ya nyumba yake na kuingia ndani kisha kuiba fedha taslimu kiasi cha Tshs 3,500,000/=, simu tano.


Aidha katika tukio hilo waliwajeruhi watu watatu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo ambao ni:-


ONESMO PAULO NYUDULA [35] Fundi Uwashi, 


THODOSIA ANTONY MGAYA [41] Mfanyabiashara na 


ADELEHEMA MUSA WANDELAGE [18] Mfanyakazi wa Ndani wote wakazi wa Mwanyanje na kisha kutoweka kusikojulika. 


Majeruhi wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na wanaendelea vizuri. Chanzo ni kujipatia kipato. Msako wa kuwatafuta na kuwakamata watuhumiwa unaendelea.


Imetolewa na:


[ULRICH MATEI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad