Jezi Mpya Yanga Zaweka Rekodi Ya Mauzo




NYOMI la watu lilijitokeza kwenye utambulisho wa jezi mpya za Yanga jana makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo Mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar.


 


Mashabiki hao waliokuwa wametinga jezi za misimu iliyopita, walionekana kuwa na shauku kubwa ya kutaka kuuona uzi wao mpya na orijino tayari kwa kuununua kwa Sh 35,000.


 


Hii ni rekodi mpya ndani ya timu hiyo kwa umati mkubwa wa watu kujitokeza kwenye uzinduzi tu wa jezi mpya kwani haijawahi kutokea.




Jezi za rangi ya kijani zenye mchanganyiko na njano mikononi na shingoni zitavaliwa nyumbani na ugenini ni njano na kaptura ya kijani na makipa watavaa za rangi ya bluu nyumbani na nyeusi ugenini, jezi zote zina ramani ya Afrika.Yanga walianza msimu huu bila ya jezi zao mpya walizokuwa wakizitumia kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kufi ka nchini kutokana na Janga la Virusi vya Corona.


 


Akizungumza na Waandishi na Habari, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela alianza kwa kuwaomba radhi mashabiki wa timu hiyo kwa kuchelewesha jezi hizo kwa muda wa wiki mbili kutokana na Corona.




Mwakalebela alisema kuwa, jezi hizo walizozindua ni zimeeandana na ubora wa kikosi chao walichokisajili kwenye msimu huu akiamini kinauwezo wa kupata matokeo mazuri muda wowote, wachezaji baadhi waliowasajili ni Michael Sarpong, Tuisila Kisinda, Yacouba Songne na Carlos Fernandez ‘Carlinohs’.


 


“Nianze kwa kutoa rai kwa mashabiki wetu wa Yanga kuwa kununua jezi zetu mpya kwenye maduka tuliyoelekeza ya GSM Mall yote na klabuni pekee na wakiziona sehemu nyingine ni feki.“Ninaamini tutangeneza historia kubwa ya mauzo ya jezi zaidi ya msimu uliopita hiyo ni kutokana na ubora wa jezi zetu ambazo zimeendana na ubora wa kikosi chetu tulichokisajili chenye uwezo wa kupata matokeo mazuri muda wowote.




“Niviombe vyombo vya dola kwa maana ya Jeshi la Polisi kutupa ushirikiano mkubwa katika mauzo haya ya jezi, lengo ni kutowapa nafasi wauzaji feki wa jezi zetu hizi mpya,” alisema Mwakalebela.


 


Kwa upande wa Mkurugenzi Uwekezaji wa GSM, Injinia Hersi Said alisema kuwa: “Niwaahidi Wanayanga kuwa kila mwaka tutatengeneza jezi mpya zenye ubora kwa dizaini nzuri itakayoendana na wananchi, leo (jana) tunatambulisha jezi za nyumbani na ugenini, ninaamini watazipokea mashabiki wetu.”




Mkurugenzi wa Udhibiti na Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas naye alisema kuwa: “SportPesa kama wadhamini tunajisikia furaha mara nyingine mbili baada ya kuwaona Yanga wanatengeneza jezi zenye ubora mzuri, kuendeleza soka siyo kidogo ni kigumu kwani fedha nyingi inahitajika.


 


“Hivyo kwa kupitia mauzo hayo ya jezi, ninaamini Yanga wataweza kujiingizia kipato, kikubwa niliombe Jeshi la Polisi kwa kusaidiana na Yanga kuhakikisha wanawadhibiti wauzaji wa jezi feki.”




Aidha, katika hatua nyingine Mshauri wa timu hiyo, Senzo Mazingisa jana alizua tafrani baada kuwarushia mashabiki wa Yanga jezi mpya mara baada ya utambulisho na kusababisha igombewe na mashabiki watano kabla ya mmoja kutoa Shilingi 20,000 ili wamuachie jezi hiyo.



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad