Sehemu kubwa ya barafu imemeguka kutoka katika hifadhi kubwa ya theruji iliyosalia ya - 79N, au Nioghalvfjerdsfjorden – katika eneo la kaskazini-mashariki mwa Greenland.
Sehemu iliyomeguka inachukua karibu kilomita 110 za mraba; picha za setilaiti zinalionesha likiwa limemeguka katika vipande vidogo vidogo.
Wanasayansi wanasema kuyeyuka zaidi kwa theruji hiyo ni ushahidi wa mabadiliko ya haraka ya hali ya hewa katika eneo hilo la Greenland.
"Hali ya hewa katika kanda hiyo imekuwa ya joto kwa kiwango cha nyuzijoto 3 tangu mwaka 1980," amesema Dkt Jenny Turton.
Barafu inashambuliwa na joto kutoka juu na chini yakeImage caption: Barafu inashambuliwa na joto kutoka juu na chini yake
"Na miaka ya 2019 na 2020, kanda hiyo ilirekodi vipimo vya hali ya juu vya joto kuwahi kurekodiwa katika msimu wa majira ya joto ," alisema mtafiti wa maeneo ya ncha ya dunia katika chuo Kikuu cha Friedrich-Alexander nchini Ujerumani aliiambia BBC.
Eneo lililofunikwa na theruji katika nchi ya dunia linalofahamika kama Nioghalvfjerdsfjorden- lina urefu unaokadiriwa kuwa sawa na kilomita 80 na upana wa kilomita 20 na lina theruji au barafu inayoenea hadi Kaskazini magharibi mwaukanda wa barafu wa Greenland - ambako inamwagika kwenye ardhi hadi baharinina kuelea tena.