Kaburi la halaiki lagunduliwa katika mji wa Terhune, mji ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji wa Kahlifa Haftar.
Jeshi la Libya limekomboa mji huo baada ya kushirikiana na jeshi la Uturuki.
Muhusika wa kitengo kinachohusika na mawasiliano serikali ya Libya amezungumza kuhusu uchunguzi baada ya kugunduliwa kaburi hilo Abdulaziz al Jafari amesema kuwa idadi ya makuburi ya halaiki inazidi kuongezeka.
Idadi ya miili iliogunduliwa bado haijatolewa.
Jeshi la Libya lilianza operesheni dhidi ya vikosi vya Haftar tangu Machi 25 na Terhune na mjini Tripoli Juni 3.
Zaidi ya makaburi 11 ya halaiki yaligunduliwa katika mji wa Terhuna.
Taarifa iliotolewa na na mahakama ya kimataifa ya Juni 22 imefahamisha kuwa makaburi ya halaiki yaliogunduliwa nchini Libya taarifa zake zinachunguzwa