Taarifa za ndani za klabu ya West Ham United maarufu wagonga nyundo wa London zinaeleza kuwa Meneja wa timu hiyo David Moyes sambamba na wachezaji wawili wameambukizwa virusi vya Ugonjwa wa Corona COVID-19.
Mapema asubuhi ya leo West Ham wameutaarifu umma kuwa mchezaji Issa Diop sambamba na Josh Cullen pamoja na Meneja Moyes walibainika kuambukizwa COVID-19 baada ya vipimo kufanyika katika kujiandaa na mzunguko wa tatu wa kombe la Carabao dhidi ya Hull City hapo jana
"Timu ya madaktari walitaarifa kuhusu matokeo ya vipimo wakati timu hiyo ilipokuwa katika uwanja wa mazoezi wa London kujiandaa na mchezo wa Jumanne jioni katika mzunguko wa tatu wa Michuano ya Carabao dhidi ya Hull City. Meneja sambamba na wachezaji hao tayari wameshaachana na kambi na kurejea nyumbani."
Mwisho timu hiyo imewatakia kupona haraka, hata hivyo Meneje msaidizi Alan Irvin alikaimu majukumu ya timu hiyo na matokeo ya mchezo wa jana usiku West Ham waliibuka na ushindi wa 5-1, Sebastien Haller na Andriy Yarmolenko wamefunga mabao mawili kila mmoja wakati Robert Snodgrass akitamatisha kalamu hiyo ya magoli
Irvin amenukuliwa akisema "Majira ya saa 12:20 jioni punde tulipokea taarifa kutoka kwa daktari wetu na kutueleza kuwa watu wetu watatu muhimu katika timu wameambukizwa COVID-19 Meneja na wachezaji wawili."
TOP STORIES
CURRENT AFFAIRS
Nkurunziza afariki dunia, chanzo chatajwa
CURRENT AFFAIRS
RC Mbeya awatimua Kidato cha 5 na 6 awataka kurudi
ENTERTAINMENT
Seyi Shay ataja orodha ya wanaume alio-date nao
CURRENT AFFAIRS
Kama alivyosema Makonda ''Wameoga'' - Kamwelwe
MOST POPULAR
CURRENT AFFAIRS
Fahamu jinsi Mtwara ilivyompa Zitto uchungu
CURRENT AFFAIRS
Maalim Seif amuunga mkono Tundu Lissu
CURRENT AFFAIRS
Ndugai kutoa 'bonus' endapo Magufuli atachaguliwa
LIFE & STYLE
Wakazi wa Vijibweni, Dar wahofia Mamba baharini
CURRENT AFFAIRS
Magufuli ataja kilichowaponza Kaliua
ABOUT US
ABOUT USADVERTISEJOBSTERMS & CONDITIONSCONTACT USFREQUENTLY ASKED QUESTIONS
NETWORK
IPP MEDIAEAST AFRICA RADIOITVRADIO ONECAPITAL RADIOLOKOPROMO
© 2020 East Africa Television Limited. All Rights Reserved