KATIBU MKUU CCM AWEKA WAZI WALIVYOJIPANGA KUFANYA MASHAMBULIZI KAMPENI UCHAGUZI MKUU



KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Dk.Bashiru Ally amesema Chama hicho katika uchaguzi mkuu mwaka huu wamepanga kufanya mashambulizi ya kampeni kwa awamu sita kwa kupita maeneo yote na tayari awamu ya kwanza imekamilika,sasa wameanza awamu ya pili. 


Dk.Bashiru pia amemuomba mgombea urais kwa tiketi ya CCM na Mwenyekiti wa Chama hicho Dk.John Magufuli kuhakikisha anaendelea kushambulia kila kona kwani wapinzani wamejileta wenyewe, hivyo asiwaonee huruma. 


Akizungumza leo Septemba 14,2020, mbele ya maelfu ya wananchi wa Chato mkoani Geita, Dk.Bashiru amesema "Nipo hapa kwa ajili ya kumuombea kura mgombea wetu Dk.John Magufuli pamoja na wagombea wote wa CCM nchi nzima ili tuweze kuendelea kuongoza Taifa letu. 


"Tumemaliza raundi ya kwanza(awamu ya kwanza) na tutakuwa na raundi sita.Raundi ya kwanza tayari na leo tunaanza raundi ya pili na kila raundi itakuwa nzito.Raundi ya pili itauwa nzito kubwa kiliko raundi ya kwanza, na raundi ya tatu itakuwa nzito kuliko ya pili,"amesema. 


Wakati huo huo Dk.Bashiru amekanusha uvuvi unaoenezwa kwamba CCM inataka kushinda viti vingi vya ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka huu ili ibadili Katiba. 


"Nataka kukanusha uvumi unaotolewa na baadhi ya watu kwamba CCM inataka kushinda viti vingi vya ubunge, kwamba wakiwa wengi bungeni wabadili Katiba.Nataka niseme hapa na iwe mwisho, hao ni watu waliochokoa na kufirisika kisiasa . 


"Dk.Magufuli anaomba miaka yake mitano ili amalize miaka 10 akapumzike,hataongoza hata sekunde moja na amekuwa akisema hili mara kwa mara.Mbona hiyo setensi ni nyepesi. Na Rais nakukabidhi raundi ya pili usiwe na huruma wamejileta wenyewe, kulia na kushoto wewe nenda nao, wakienda nje wewe baki nchi endelea kuchapa kazi,"amesema Dk.Bashiru.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad