No title



KATIBU  Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),  John Mnyika,  amesema chama hicho kimeiandikia barua Tume ya Uchaguzi ya Taifa (NEC) ili  kuainisha kwa kina rufaa zilizotolewa na wagombea na zilivyofanyiwa maamuzi pamoja na kuiomba kuwachukulia hatua wasimamizi wa uchaguzi katika majimbo kwa kuwaengua wagombea bila kufuata utaratibu

Mnyika ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 14, 2020, jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema majimbo ya Butiama, Handeni Vijijini, Kavuu, Kwimba, Kondoa Vijijini, Gairo, Morogoro Mjini, Songwe, Ludewa, Msalala, Lupa ni miongoni mwa majimbo ambayo uamuzi wake haujatolewa.

“CHADEMA imekata rufaa zaidi ya 400 za udiwani lakini mpaka sasa ni rufaa 100 tu ambazo zimetolewa maamuzi, suala ambalo linaminya demokrasia.  Kwa mfano jimbo la Ukerewe msimamizi wa uchaguzi ameanza kuengua wagombea wa udiwani ambao hawakuwekewa pingamizi,” amesema Mnyika.

Kutokana na maamuzi hayo yaliyofanywa na msimamizi wa Jimbo la Ukerewe, CHADEMA imeiomba tyume kumchukulia hatua stahiki

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad