Kenya yakiri Vifurushi 21 vya msaada wa matibabu ya Corona, kutoka kwa bilionea Jack Ma havikufika Bongo5 · Ally Juma · 50 minutes ago Kenya imekiri kuwa mchango muhimu katika kupambana na #COVID19 kutoka kwa Bilionea wa China, Jack Ma haukuwasili nchini humo. Naibu wa Waziri wa Uchukuzi Nchini humo, Chris Obure amesema vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vimeonekana kutofika baada ya kuthibitisha katika stakabadhi za kuhifadhi kutoka China. Vifaa hivyo viliwasili Ethiopia lakini katika usambazaji ndipo havijulikani vilipokwenda. Ethiopia ilikuwa ni nchi iliyopewa msaada ili kusambaza kwa nchi nyingine za Afrika. Hata hivyo, hivi karibuni Kenya imekumbwa na kashfa ya ubadhirifu dhidi ya misaada ya #COVID19 ikiwemo kutumiwa vibaya au kupotea katika njia za kutatanisha. Naibu wa waziri wa uchukuzi wa Kenya, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya. Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure. Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha. OPEN IN BROWSER



Kenya imekiri kuwa mchango muhimu katika kupambana na #COVID19 kutoka kwa Bilionea wa China, Jack Ma haukuwasili nchini humo.



Naibu wa Waziri wa Uchukuzi Nchini humo, Chris Obure amesema vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vimeonekana kutofika baada ya kuthibitisha katika stakabadhi za kuhifadhi kutoka China.


Vifaa hivyo viliwasili Ethiopia lakini katika usambazaji ndipo havijulikani vilipokwenda. Ethiopia ilikuwa ni nchi iliyopewa msaada ili kusambaza kwa nchi nyingine za Afrika.


Hata hivyo, hivi karibuni Kenya imekumbwa na kashfa ya ubadhirifu dhidi ya misaada ya #COVID19 ikiwemo kutumiwa vibaya au kupotea katika njia za kutatanisha.


Naibu wa waziri wa uchukuzi wa Kenya, Chris Obure amefichua kuwa vifurushi 21 vilivyokuwa na vifaa vya matibabu vilivyotolewa na wakfu wa Jack Ma mwezi Machi kama msaada wa kukabiliana na Covid 19 haikufika Kenya.




Wizara ya uchukuzi iligundua kuwa vifurushi 21 havikuwepo baada ya kuthibitisha hilo katika stakabadhi za kuegesha kutoka China.‘’Binafsi niliongea na maafisa wakuu wa Wizara ya Afya na walinithibitishia kuwa wanafuatilia suala hilo’’ alisema bwana Obure.


Kumekuwa na madai kwamba misaada ya Covid-19, ikiwemo ile kutoka kwa Ma ilitumiwa vibaya au kutoweka katika njia za kutatanisha.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad