Kenya yatoa orodha ya majina ya watu 9 na kuzuia mali zao, wakielezwa kufadhili kundi la kigaidi Al Shabab



Wizara ya Mambo ya Ndani ya Kenya imetoa orodha ya majina ya watu tisa iliosema wanafadhili shughuli za kundi la kigaidi, Al-shabaab nchini humo, na kuamuru kushikiliwa kwa fedha na mali zao. Kundi hilo limekuwa likitekeleza mashambulizi yaliyoua mamia ya watu nchini Kenya.



Wizara ya mambo ya ndani imesema hatua hiyo ni sehemu ya juhudi mpya za kukabiliana na ugaidina  ugaidi nyumbani’’

Katika taarifa yake waziri wa usalama wa kitaifa Fred Matiangi amesema kuzuiliwa kwa mali ya Wakenya hao tisa kutahakikisha hawawezi tena kufadhili kundi la Al Shabab ‘’ ndani ya mipaka yetu’’.

Pia ameonya kuwa kundi hilo lilikuwa likiwasajili ,kuwapa mafuzo na kuwawekamiongoni mwa raia‘’ ili waendeleze ajenda yao ya misimamo mikali na ugaidi.”

Tangazo hilo linajiri wakati ambapo Rais Uhuru Kenyatta amewaambia viongozi wa kimataifa kwamba janga la Covid 19 limechangia vitendo vya kigaidi, kuzidisha mzozo wa wakimbizi na kuongezeka kwa silaha ndogo ndogo katika eneo la Pembe ya Afrika.

Kenya imekabiliwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa Al Shabab tangu ilipowapeleka wanajeshi wake Somalia 2011 kukabiliana na kundi hilo

Rais Kenyatta ailikuwa akizungumza katika mkutano wa Aqaba kuhusu Covi-19 uliandaliwa kupitia mfumo wa kidijitali na Mfalme Abdullah wa pili wa Jordan ambao pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, Rais Rodrigo Duterte wa Ufilipino na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress kujadili jannga la corona na usalama wa kimataifa.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad