Kikongwe wa miaka 99 apokea fidia ya mamilioni

 


kikongwe Nasi Muruo 99 mkazi wa Sinoni Arusha amepokea kiasi cha fedha shilingi milioni 246.2 kama fidia kutoka katika kaya 76 baada ya Rais Magufuli kuingilia kati mgogoro wa ardhi aliyonyang’anywa kikongwe huyo tangu mwaka 1977na kushinda kesi mwaka 1979 lakini hakurudishiwa.


Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Wiliamu Lukuvi, Agosti 28,mwaka 2019 aliamuru kaya 110 zilizojengwa kwenye ardhi ya kikongwe huyo kumlipa fidia ya shilingi millioni 519 kulingana na ukubwa wa kila nyumba vinginevyo zitabomolewa.


“Nashukuru kaya ambazo zimeanza kunilipa, namshukuru Rais Magufuli na waziri Lukuvi nimenza kupata haki yangu baada ya kuitafuta kwa miaka 43”. Amesema Muruo.


Mjukuu wa Bibi Muruo Obedi Saiteru ameiomba familia iliyosababisha mgogoro huo kuondolewa kwaa kuwa imeanza kampeni ya kushawishi watu wasikamilishe malipo na kuendeleaa kung’ang’ania ardhi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad