Kim jong-un aomba msamaha wa mauaji ya afisa wa Korea Kusini

Kim jong-un aomba msamaha wa mauaji ya afisa wa Korea Kusini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ameomba msamaha kufuatia mauaji ya afisa wa Korea Kusini, kwa mujibu wa ofisi ya rais Korea Kusini.

Bw Kim ameripotiwa kumwambia mwenzake wa Korea Kusini Moon Jae-in kwamba tukio hilo halikustahili kufanyika.


Korea Kusini inadai mtu huyo mwenye umri wa miaka 47-alikuwa akijaribu kutoroka kutoka Korea Kaskazini alipopatikana na wanajeshi wa nchi hiyo walikuwa wakishika doria.


Baada ya hapo alipigwa risasi na mwili wake kuteketezwa moto, kulingana na Seoul.


Mpaka kati ya Korea hizo mbili unalindwa vikali na Kaskazini inasadikiwa kutekeleza sera ya "kuua kwa kupiga risasi" kumzuia asiingize virusi vya corona nvhini mwao.


Msamaha huo ulitolewa kupitia njia ya barua iliyotumiwa Rais Moon kuelezea kuwa tukio hilo halikustahili kufanyika, kwa mujibu wa afisa mmoja.


Bw.Kim alisema a "naomba msamaha" kwa "kuwakosea" Bw Moon, iliripoti shirika la habari la Yonhap, likinukuu Blue House.


Kaskazini pia ilitoa maelezo zaidi kuhusubtukio hilo, ikisema mtu huyo alipigwa risasi kumi.


Pia ilifafanua kuwa haikuchoma mwili wa mtu huyo bali ni "kifaa kilichokuwa kinaolea majini" ambacho kilitumia kumbeba,mkurugenzi wa usalama wakitaifa wa Kusini Suh Hoon.



Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad