Mwanamitindo maarufu nchini Marekani Kim Kardashian ametangaza kufunga akaunti zake za mitandao ya kijamii ya Instagram na Facebook kwa sababu ya maneno ya chuki yanayosambaa mitandaoni.
Taarifa hiyo ya kufunga akaunti zake ametangaza kwenye mtandao wa Twitter ambapo ameandiaka kuwa
"Siwezi kukaa kimya wakati mitandao ikiendelea kuridhia kusambaza kwa habari za chuki, propaganda na taarifa zisizosahihi zilizizoandaliwa na makundi yanayotaka kuingawa Marekani"
Hatua hiyo ni sehemu ya Kampeni za kupinga chuki inayojulikana kama waache chuki kwa faida 'Stop hate for profit' ambayo imeandaliwa na wanaharakati wa haki za Raia, pia Katy Perry ameunga mkono uamuzi huo wa Kim Kardashian kuhusu maneno yanayosambaa mitandaoni.
Aidha muanzilishi wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa watapiga marufuku matangazo yaliyo na madai ya aina hiyo na kuongeza kuwa tayari wamejiandaa kukabiliana na hali hiyo kabla ya kufikia uchaguzi