Kim Kardashian West na wasanii wengine wametangaza kufunga akaunti zao za mitandao ya kijamii kupinga kuenea kwa chuki kwa chuki, propaganda na taarifa zisizo sahihi".
"Taarifa potofu zinazowekwa mitandaoni zina athari kubwa," Kardashian West aliandika siku ya Jumanne.
Hatua hiyo ni sehemu ya kampeni ya kupinga chuki ifaamikayo kama #StopHateforProfit ambayo imeandaliwa na wanaharakati wa haki za raia.
Wasanii hao watafunga akaunti zao za mitandao ya kijamii kwa muda 24 , siku ya Jumatano.
"Siwezi kukaa kimya wakati mitandao ikiendelea kuridhia kusambazwa kwa habari za chuki , propaganda na taarifa zisizosahihi- zilizoandaliwa na makundi yanayotaka kuigawa Marekani , alisema," Kardashian West said.
"Upotoshaji wa taarifa unaotumwa mitandaoni una athari kubwa katika uchaguzi na kuminya demokrasia yetu," aliongeza.
Wasanii wengine ambao wamekubali kushiriki katika zoezi hilo ni pamoja na waigizaji Leonardo DiCaprio, Sacha Baron Cohen na Jennifer Lawrence,pamoja na muimbaji Katy Perry,
"Siwezi kukaa tu bila kufanya kitu wakati mitandao ya kijamii inafumbia macho makundi ya watu wanaotuma ujumbe na maoni ya chuki na yasio na ukweli wowote," Perry aliandika katika mtandao wa Instagram.
Muigizaji Ashton Kutcher, ambaye ana mamilioni ya wafuasi pia amejiunga katika kampeni hiyo , alisema mitandao hii haikutengenezwa ili kusambaza chuki na ghasia".
Waandaaji wa kampeni ya #StopHateforProfit campaign, ambayo ilizinduliwa Juni , imeishutumu Facebook na Instagram kwa kushindwa kusitisha taarifa za chuki na za upotoshaji.
Kundi hilo limewalenga Facebook, ambayo pia inamiliki Instagram na WhatsApp na mwaka jana kampuni hiyo iliweza kupata kodi ya matangazo ya karibu dola bilioni sabini $70bn (£56.7bn).
Maelfu ya biashara na makundi ya kutetea haki za raia yalisaini kampeni hiyo.
"Tunakaribia kufikia uchaguzi mmoja ambao ni muhimu sana katika historia ya Marekani," kundi hilo liliandika katika taarifa yake.
Mwezi Juni, Facebook ilisema kuwa itaweka alama kwenye machapisho ambayo yangeweza kuwa na madhara au yanapotosha watu.
Muasisi wa Facebook, Mark Zuckerberg alisema pia kuwa kampuni ya mitandao ya kijamii itapiga marufuku matangazo yaliyo na madai ya aina hiyo "kuwa watu wa kabila Fulani, asili yao, taifa , mitazamo ya dini , jinsia na nyinginezo ni tishio kwa wengine.
"Tayari tulikuwa tumejiandaa kukabiliana na hali hiyo katika uchaguzi wa mwaka 2020," aliandika katika taarifa yake. "Katika wakati huu, Facebook itachukua tahadhari zaidi ili kusaidia kila mtu awe salama na kupata taarifa sahihi."
Lakini kampeni ya #StopHateforProfit inataka jitihada zaidi kufanyika kukabiliana na tatizo hilo na huku zaidi ya makampuni 90 yamesitisha matangazo yao kuunga mkono jitihada hizo.
Matokeo ya hatua hiyo ya kususia mitandao, hisa za Facebook zilishuka ghafla na vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa dola bilioni 7.2 ziliondolewa katika fedha binafsi za Zuckerberg.
Watunga sheria na wasimamizi walioko duniani wana wasiwasi kuhusu kukua kwa ongezeko la taarifa za chuki, sio kwenye mitandao ya Facebook peke yake ,katika mataifa mengi wanaibua maswali ya namna teknolojia inavyofanya kazi na jinsi inavyokabiliana na tatizo .