Kimenuka...Wanajeshi 9 wa Afghanistan wauwawa



Kumekuwa na mashambulio mabaya nchini Afghanistan leo licha ya majadiliano kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan na wakati dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya amani. 



Katika moja ya mashambulizi yaliyosababisha maafa makubwa, wanamgambo wa taliban wamewauwa wajeshi tisa wa jeshi la Afghanistan usiku katika jimbo la kaskazini la Takhar. 




Mashambulizi hayo yanakuja wakati pande hizo mbili zinajadili misingi ya amani nchini Afghanistan, mazungumzo yanayofanyika katika nchi ya Qatar. 

Mjumbe wa Marekani kwa ajili ya maridhiano ya Afghanistan, Zalmay Khalilzad, ambaye ametayarisha mazungumzo hayo, amesema kuwa hali hiyo ya kuongezeka kwa mashambulizi kuwa inasikitisha. Mwenyekiti wa baraza la juu la taifa la maridhiano, Abdullah Abdullah , amelitaka kundi la Taliban kukubali kusitisha mapigano.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad