Kisa Corona Kuzidi...Boris Johnson kuwataka Waingereza kufanyia kazi nyumbani



Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anatarajiwa kutangaza masharti mapya ya kudhibiti ongezeko la maambukizi ya COVID-19, wakati nchi hiyo ikishuhudia wimbi la pili la kusambaa kwa kasi kwa ugonjwa huo. 


Miongoni mwa masharti atakayoyatangaza ni kuwataka wakaazi wa Uingereza kufanya kazi nyumbani badala ya ofisini, na kufupishwa kwa muda wa huduma katika baa na mikahawa. 


Katika ujumbe wake wa vidio uliorikodiwa, Johnson ataliambia taifa lake kuwa mipango hiyo mipya ni migumu, lakini inahitajika ili kudhibiti kuongezeka kwa visa vya maambukizi, na kuilinda huduma ya afya ya nchi hiyo, NHS. 


Wiki chache tu zilizopita serikali ya Johnson iliwahimiza Waingereza kurejea kazini kama kawaida, lakini imebadilisha kauli baada ya kuongezeka haraka kwa idadi ya wagonjwa wa COVID-19 wanaokwenda hospitali kutafuta matibabu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad