Mtangazaji Diva amemueleza msanii Marioo asifikie hatua ya kujinyonga kisa mapenzi, atualie na atapata mwanzake mzuri kwa ajili yake.
Wikiendi iliyomalizika #Marioo amegonga vichwa vya habari mtandaoni mara baada ya kuposti picha ya kitanzi, huku akieleza kuumizwa na mapenzi.
“Najua mapenzi yanauma sana ila nakusihi kama Mama yako usijinyonge mademu wako wengi sana utapata tu mwengine, nakupigia tuongee yaani usije jaribu. I have been in the situation where by unaona maisha tena basi hilo ni miaka imepita uko enzi zangu za ujana ila unaangalia pia maisha na kwanini upo,” ameeleza Diva.
Ameendelea kwa kusema, “Ukijua thamani yako na wewe ni nani basi huwezi hiko la kitanzi mwanangu, healing is a process utapona tu and life goes on, suala la mapenzi my son bora uhai,”