Kodak Black "Trump Naomba Unitoe Gerezani"


Kodak Black ameendelea kupaza sauti juu ya kifungo chake, jana imetoka taarifa kwamba amemuomba Rais Trump kumtoa gerezani.


Timu ya wanasheria wa rapa huyo ikiongozwa na Bradford Cohen na Jonathana Schwartz wametuma hati ya pingamizi (petition) kwa Rais Trump wakimuomba aweze kumsaidia kumtoa gerezani. Kwenye maelezo yake Cohen amesema Kodak anatumikia kifungo cha miezi 46 gerezani kwa makosa ya silaha, huku kiwango cha kawaida cha hukumu ya makosa hayo ni miezi 18.


Wiki hii Kodak alizungumza na kusema amefungua mashtaka dhidi ya mamlaka ya magereza kwani amekuwa akipitia changamoto ya kupigwa na kuteswa gerezani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad