Korea Kaskazini yadaiwa kumuua raia wa Korea Kusini aliyevuka bahari

 


Serikali ya Korea Kusini imesema afisa wa Serikali aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha akiwa anavua samaki katika eneo linalopakana na nchi jirani ya Korea Kaskazini amepigwa risasi na askari wa nchi jirani.


Habari zinasema boti ya Afisa huyo kutoka Korea Kusini, ilisukwa sukwa na mawimbi na kujikuta imevuka mpaka wa bahari na kuingia katika eneo la bahari la nchi jirani ya Korea Kaskazini.


Askari wa nchi hiyo walimshambulia kwa risasi kadhaa ambazo zilisababisha majeraha makubwa katika mwili wake na kisha kumsababishia mauti.


Korea Kusini imesema mwili wa afisa huyo umekutwa ukiwa umechomwa moto licha ya kuwa na majeraha ya risasi, hali ambayo imeanza kusababisha fukuto la uhusiano wa kimataifa kati ya mataifa hayo mawili jirani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad