Korea Kaskazini imesema ilikuwa inautafuta mwili wa raia wa Korea Kusini aliyeuwawa na wanajeshi wake, lakini ikionya kwamba shughuli za kijeshi za Korea Kusini zilitishia kuongezeka kwa wasiwasi.
Kulingana na shirika la habari la habari la Korea Kaskazini, KNCA hii leo mamlaka za nchini humo zilikuwa zinazingatia namna ya kuukabidhi mwili huo kwa Korea Kusini iwapo utapatikana.
Ripoti ya KNCA ililiita tukio hilo kuwa ni baya na ambalo halikutakiwa kutokea ingawa ilionya kwamba shughuli za kijeshi za Korea Kusini karibu na eneo kulikotokea tukio hilo zilikuwa zimevuka na kuingia kwenye eneo la maji ya Korea Kaskazini na kutaka kusimamishwa kwa shughuli hizo ili kuepusha hali ya wasiwasi.
Msemaji wa wizara ya ulinzi ya Korea Kusini alipoulizwa alisema hawezi kuzungumzia tuhuma hizo za Korea Kaskazini kwa sasa.