Mwanasaikolojia na Mshauri Mahusiano Chris Mauki amesema kuwa kwenye mahusiano na mtoto wa mwisho kwenye familia ni shida sana kwani wamezoea na kutaka kufanyiwa kila kitu.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Chris Mauki amesema uki-date na watoto wa mwisho unaweza ukadhani kama umeoa familia nzima jinsi utakavyomfanyia mtoto wao.
"Oda ya kuzaliwa ina ishu sana matokeo yake wanashindwa kukabiliana nayo, kwenye jamii mtoto wa kwanza anakuwa kiongozi na kufundishwa kufanya maamuzi, mtoto wa pili anakuwa kama ana-loose kitu kisa mtoto wa kwanza yupo, anayefuatia anakuwa yupo cool sana anapatanisha watu wakikosana, ila wa mwisho wanakuwa hawajishughulishi wanapenda kufanyiwa pia wanakuwa na hisia sana"
"Ukidate na mtoto mwisho kwenye famili Utashangaa ukimuona kwenye mahusiano utadhani kama umeoa familia nzima akionekana vibaya utasemwa wewe akikonda utaulizwa wewe au usipompa maziwa utaulizwa wanakuaga na shida sana hii"
Pia ameongeza kusema kama wakikutana mtoto wa mwisho na wa mwisho mwenziye kwenye mahusiano yao wanaweza wasifanye maamuzi na wanaweza hata wasijenge kabisa.