Maafisa saba wa polisi wamesimamishwa kazi nchini Marekani, kuhusiana na madai kwamba polisi walitumia nguvu dhidi ya Mmarekani mwingine mweusi.
Meya wa mji wa Rochester katika jimbo la New York, Lovely Warren ametangaza hatua hiyo. Siku moja kabla ya tangazo hilo, ndugu wa mhanga huyo walichapisha mtandaoni vidio iliyoonyesha operesheni ya polisi iliyofanyika mwishoni mwa mwezi Machi, ambapo polisi mmoja alionekana akimfunika mfuko kichwani Mmarekani mweusi Daniel Prude, aliyekuwa amepiga magoti, akiwa mtupu huku akiwa amefungwa pingu mikononi.
Polisi wamejitetea kwa kusema kuwa lengo la kufanya hayo lilikuwa ni kumzuia Prude kuwatemea mate. Mmarekani huyo mweusi Daniel Prude mwenye umri wa miaka 41 alifariki hospitalini wiki moja baada ya tukio hilo.