Kikao cha Kamati ya Maadili ya Mawakili kilichoitishwa na Chama cha Wanasheria wa Tanganyika, TLS kilichoketi leo, Septemba 23, 2020 kimeamuru kuondolewa kwa jina la Fatma Karume katika orodha ya mawakili Tanganyika kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kutokana na kukutwa na hatia ya kukiuka maadili ya kazi yake.
Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Karume kufukuzwa kwenye Kampuni ya Mawakili ya IMMMA Advocates alikokuwa akifanya kazi kwa kipindi kirefu.