Majibu yaliyopatikana baada ya Watalamu kufanya utafiti kuhusu Binadamu kunywa pombe wakati wa kula naona yatawafurahisha Wanywaji wengi wa pombe kwani imeonekana kufanya hivyo wakati wa kula kuna faida.
Utafiti huo uliochapishwa kwenye Journal Epidemiology umeeleza kwamba kunywa pombe kidogo huku unakula chakula kunasaidia kukata sumu kwenye chakula haijalishi ni sumu gani, yaani iwe iliyowekwa makusudi kwenye chakula au sumu zinazotokana na chakula kutopikwa vizuri au kuingia vijidudu.
Utafiti huo umeeleza kwamba sumu zote hizo zitakatwa au kuondolewa na funda moja au mbili za pombe wakati wa kula lakini Watafiti hao wakasisitiza kwamba hata hivyo majibu haya hayamaanishi kwamba Watu ndio wawe wanabwia pombe kwa wingi wakati wa kula.
“Hatusemi Watu wabugie pombe kama wanafanya mashindano kwani hata ladha ya chakula itakata, wanywe kistaarabu funda moja au mbili zinatosha” – Journal Epidemiology