Moja ya eneo kubwa lenye mkusanyiko wa nyenzo nyingi za matandaoni za kundi la Islamic Stale limebainika na watafiti katika Taasisi ya majadiliano ya Kimkakati.
Maktaba hiyo ya mtandaoni ina nyenzo zaidi ya 90,000 na inasemekana wageni wanaoitembelea kwa mwezi idadi yao inakadiriwa kuwa 10,000.
Wataalamu wanasema maktaba hiyo imewezesha kundi hilo lenye msimamo mkali kubadilisha na kuongeza maudhui yake mtandaoni.
Lakini kuondoa maktaba hiyo ni changamoto kwasababu data hiyo haihifadhiwi sehemu moja.
Licha ya hatua za kukabiliana na ugaidi, Uingereza na Marekani zimetahadharishwa kuhusu maktaba hiyo inavyozidi kupanuka.
Ugunduzi wa maktaba hiyo umewadia baada ya kufariki dunia kwa kiongozi maarufu Abu Bakr al-Baghdadi, Oktoba 2019.
Wakati huo, ujumbe mwingi wa mitandao ya kijamii unaounga mkono shirika ukiwa na viunganishi vifupi
Viunganishi hivyo vimesaidia watafiti kufikia nyaraka na video zilizohifadhiwa kwa lugha tisa tofauti.
Walijumuisha taarifa za mashambulizi ikiwemo yaliyotekelezwa katika maeneo ya Manchester Mei 22, 2017, na Uingereza Julai 2005 na Marekani September 2001.
"Kuna kila kitu unachohitajika kujua ili kupanga shambulio," amesema naibu mkurugenzi wa Taasisi ya Majadiliano ya Kimkakati Moustafa Ayad, aliyefumbua hifadhi hiyo.