Mama mjamzito amuokoa mumewe kutoka katika mdomo wa Papa



Mwanamke mja mzito aliogelea baharini katika eneo la Florida kumuokoa mumewe aliyekuwa anashambuliwa na papa.




Maafisa wa polisi walisema kwamba Andrew Charles Eddy 30, alikuwa akiteleza baharini kwa kutumia ubao katika eneo la Sombrero ndipo akaumwa na papa mara tu alipoingia baharini.


”Mkewe aliuona mgongo wa papa huyo huku damu ya mumewe ikianza kutapakaa baharini na kuruka baharini bila kusubiri”, maafisa wanasema.


Baada ya kumuokoa mumewe na kumpeleka eneo salama ndugu zake wengine walipiga simu kwa 911 kupata usaidizi. Alisafirishwa kwa ndege hadi katika kituo cha kukabiliana na majeruhi ambapo alitibiwa jeraha baya la bega.




Afisa wa uokozi Ryan Johnson aliambia vyombo vya habari kwamba bwana Eddy alikua katika hali mbaya wakati alipowasili.


Wanandoa hao kutoka jimbo la Georgia, walikuwa katika likizo katika jimbo la Florida na familia na walikuwa wakisafiri kwa kutumia boti la binafsi pamoja.


Baadhi yao walikuwa tayari wakiteleza baharini kwa kutumia ubao wakati bwana Eddy alipoingia baharini kujiunga nao.


Naibu Christopher Aguanno aliandika katika ripoti ya polisi kwamba kulikuwa na watu wengine wasiotoka katika kundi lao waliokuwa wakiteleza kwa ubao baharini.


Mashahidi baadaye waliripoti kumuona papa mkubwa mwenye urefu wa futi 10 akiogelea katika eneo hilo mapema siku hiyo.


Florida ina idadi kubwa ya mashambulizi ya papa duniani, huku visa 21 vikiripotiwa 2019 kulingana na makavazi ya Florida.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad