IMEFAHAMIKA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mserbia Zlatko Krmpotic bado hajachagua nahodha wa kikosi chake ambacho kesho kitajitupa kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Wachezaji wanaovaa kitambaa cha unahodha hivi sasa kwa kubadilishana katika michezo mitatu ya ligi waliyocheza ni Deus Kaseke, Haruna Niyonzima na Lamine Moro.
Kabla ya ujio wa Zlatko, Kaseke ndiye aliyekuwa amepewa majukumu yaliyoachwa na Mkongomani Papy Tshishimbi huku Niyonzima akiwa msaidizi wake.Kwa mujibu wa taarifa nahodha huyo na wachezaji wanaopigiwa chapuo ni Niyonzima na Moro.
“Kikubwa kocha anamtaka nahodha atakayekuwa kiunganishi kati ambazo Championi Jumamosi limezipata, Zlatko ameshindwa kuamua nani ampe unahodha kutokana na kila mmoja kutojihakikishia nafasi ya kucheza katika kikosi chake cha kwanza wakati akiendelea kuisuka timu yake.
Mtoa taarifa huyo alisema kuwa licha ya kocha huyo kutoamua unahodha uende kwa nani, lakini amechagua majina mawili Niyonzima na Moro ambayo hivi sasa anayapambanisha katika kumpata mmoja atakayekiongoza kikosi chake.
Aliongeza kuwa cheo cha nahodha ni kikubwa katika timu hivyo anataka kumpa mchezaji atakayekuwa kiongozi wa wachezaji wenzake na kiunganishi kati ya wachezaji na uongozi.
“Kocha bado hajampata nahodha mkuu atakayeiongoza timu, hivi sasa yupo katika hatua za mwisho za kumpata ya wachezaji na uongozi, pia atakayeiongoza timu itakapokuwa uwajani ikicheza mechi zake.
“Kigezo kingine anachokiangalia kocha ni uwezo wa kuongea lugha zaidi ya mbili ambazo ni Kiingereza Kiswahili na Kifaransa hiyo ni kutokana na timu yao kuundwa na wachezaji wa mataifa mbalimbali wanaozungumza lugha hizo,” alisema mtoa taarifa huyo.
Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema: “Hilo jukumu siyo letu ni la benchi la ufundi ambalo lipo chini ya kocha Zlatko, sisi tunahusika na masuala ya kiutawala pekee.