Mbelgiji Amaliza Utata wa Bocco na Kagere


RASMI Kocha Mkuu wa Simba Mbelgiji, Sven Vandenbroeck amemtangaza nahodha wa timu hiyo, John Bocco ndiye chaguo lake la kwanza katika kikosi chake cha kwanza katika msimu huu mpya wa Ligi Kuu Bara 2020/2021.

Kwa maana hiyo mfungaji bora mara mbili mfululizo Mnyarwanda, Meddie Kagere na mshambulijai mpya Mkongomani, Chris Mugalu aliyetokea Klabu ya Lusaka Dynamos ya nchini Zambia hawana nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza.

 
Kagere alichukua ufungaji bora msimu wa 2018/2019 ambao alifanikiwa kufunga mabao 23 kabla ya msimu uliopita wa 2019/2020 akipachika mabao 22 pekee.

Kwa mujibu wa Sven, mshambuliaji wake Bocco ndiye aliyekuwepo kwenye kiwango kizuri hivi sasa katika kikosi chake, hivyo haoni sababu ya kumuweka benchi na kumpanga mchezaji mwingine.


Sven alisema kuwa, anafurahishwa na aina yake ya uchezaji ya Bocco ambayo imemshawishi aendelee kumtumia katika msimu ujao kama mshambuliaji mmoja kutokana na aina ya mfumo anaoutumia.

Aliongeza kuwa licha ya kumpa nafasi Bocco, lakini anaamini hao wengine waliokuwepo Kagere na Mugalu bado anaamini uwezo wao wa kufunga mabao katika timu.

“Ninaamini uwezo wa washambuliaji wangu wote waliokuwepo katika timu, lakini mara nyingi nimekuwa nikimpa nafasi mchezaji yule aliye kwenye kiwango bora katika timu.


“Hivyo, basi kwa hivi sasa mshambuliaji aliye bora ni Bocco kwani anatimiza majukumu yake vizuri ikiwemo kucheza kwa kufuata maelekezo yangu,” alisema Sven.

Simba, leo inatarajiwa kufungua pazia la ligi kwa kucheza na Ihefu FC ya Mbarali, Mbeya mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine mkoani huko.

Stori: Wilbert Molandi, Dar es salaam
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad