Kwa mujibu wa mtandao wa Goal.com, Mshambuliaji wa Aston Villa Mbwana Samatta amewasili katika mji wa Istanbul ili kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kwa klabu ya Fenerbahce.
Adios to that flop' - Many Aston Villa fans react as £9.45m-valued misfit looks set to depart | The Transfer Tavern
Nyota huyo raia wa Tanzania mwenye umri wa miaka 27 alijiunga na Villans akitokea Genk mwezi Januari na kufunga jumla ya magoli mawili pekee kwenye michezo 16 aliyocheza chini kocha Dean Smith.
Mara kadhaa klabu ya Fenerbahce imekuwa ikihusishwa kuhitaji saini ya mshambuliaji huyu hatariwa Taifa Stars tangu walipoona hatma yake ndani ya Villa sio nzuri.
Hata hivyo West Bromwich Albion walikuwa pia wakihusishwa na mchezaji huyo ambaye kwa sasa inadaiwa tayari ameshartua katika jiji la Instanbul kukamilisha dili hilo la mkopo wa mwaka mmoja na Fenerbahce huku wakiwa wanayo nafasi ya kumnunua moja kwa moja.