MSHEREHESHAJI maarufu nchini Saleh Kumbuka a.k.a Dk kumbuka amepata ubalozi wa kampuni ya Magic Corporation, kwa bidhaa ya dawa ya mbu ijulikanayo kwa jina la My Comfort.
Akizungumza na Michuzi tv amesema anashukuru kampuni hiyo kwa kumuamini kumpatia ubalozi wa kazi zao.
"Nashuru kwa kupata nafasi hii adhimu ambayo watu wengi wanaitamani dawa ya My Comfort nimeshaitumia nimeona ubora wake hivyo niombe jamii yangu kuitumia ili kujikinga na maradhi."
Pia ametoa rai kwa watu maarufu kujijengea heshima mbele ya hadhira ili kuwapa Moyo makampuni,taasisi na mashirika kuona ipo haja ya wao kuwapa ubalozi ili kusupport kazi zao.
"Heshima na nidhamu yangu imefanya nipate huu mchongo na kwa Sasa itambulike kuwa nimepata ubalozi wa miaka miwili,nitatangaza kila Kona dawa hi ya mbu "my comfort."