MELANIA TRUMP; KUTOKA UANAMITINDO HADI KUWA MKE WA RAIS



MWANAMITINDO, Mfanyabiashara na Mke wa Rais wa 45 wa Marekani Donald Trump anafahamika kwa jina la Melania Trump, alizaliwa Aprili 26, 1970 na kukulia Novo Mesto kwa sasa Slovenia na kupewa  jina la Melanija Knavs, alisoma katika Chuo kikuu cha Ljubljana, Yugoslavia Slovenia kwa sasa ambako hakumaliza masomo yake baada ya kuegemea zaidi katika fani yake ya ulimwende.


Melania alianza kujihusisha na urembo akiwa na miaka 16 tuu, Mama yake alikuwa mbunifu wa nguo za watoto na baba yake alijihusisha na biashara za magari, na alibadili herufi za jina lake kutoka Melanija Knavs na kuwa Melania Knaus alipoingia katika fani ya urembo aliyoifanya kupitia mawakala wa Milan Paris kabla ya kuhamia Marekani. 


Licha ya kutozungumza Kiingereza kama lugha ya kwanza Melania anazungumza kwa ufasaha lugha sita ambazo ni Kislovenia, Kifaransa,Kiitaliano, Kisebia, Kijerumani na Kingereza.


Melania ni 'First Lady' wa pili ambaye amezaliwa nje ya Marekani katika historia ya nchi hiyo baada ya Louisa Adams aliyezaliwa Uingereza na kuwa mke wa Rais wa sita wa nchi hiyo John Quincy Adams aliyehudumu 1825-1829.


Alihamia Newyork, Marekani mwaka 1996 kwa shughuli za ulimwende na alifanya kazi kwa karibu na wapiga picha maarufu wakiwemo Helmut Newton na Demarchelier Patrick na kutokea katika magazeti mbalimbali likiwemoHarper's Bazaar la nchini Bulgaria.


Alibahatika kukutana na Donald Trump mwaka 1998 katika tafrija ya mitindo katika ukumbi wa Kit Kat Club, mjini Newyork na ilipofika 2004 walihalalisha uchumba wao.


 Ilipofika Julai, 2006 licha ya Melania kupata uraia kamili wa nchi hiyo pia walibarikiwa mtoto wa kiume Barron William Trump, huku akiwa mke wa tatu kwa Trump, Awali Trump alimuoa Ivana Trump hadi 1992 na Marla Maples hadi mwaka 1999, Licha ya kuwa First Lady Melania ni Mfanyabiashara wa

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad