Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Tanasha Donna Oketch, ameponzwa na meneja wake ajulikanaye kwa jina la Jamal Gadaffi.
Hayo yamejiri siku chache baada ya kuwepo kwa tetesi za memba wa lebo kubwa ya muziki Bongo ya Wasafi Classic Baby (WCB), Zuhura Othman ‘Zuchu’ kukopi baadhi ya mashairi ya ngoma yake ya Cheche kutoka kwa Tanasha.
Tanasha amejikuta akishambuliwa na baadhi ya mashabiki kutokana na kile kilichofanywa na meneja wake huyo na kusababisha ngoma hiyo kushushwa au kuondolewa kwenye Mtandao wa YouTube.
Mashabiki hao wamekuwa wakimshambulia Tanasha mitandaoni kutokana na sakata hilo lililofanywa na Jamal ikiwa ni baada ya kuposti kipande cha Wimbo wa Cheche na wa Usher Raymond, japo aliifuta baada ya muda mfupi.
“Mbona kama meneja wa Tanasha anatufuatilia sana na vijembe vinazidi kuwa vingi na kutengeneza chuki?’’ Aliandika mmoja wa mashabiki hao kwenye Mtandao wa Instagram.
Tanasha na Zuchu wameingia katika sakata hilo ikiwa ni baada ya kugundulika kuwa Zuchu amekopi baadhi ya mistari kwenye ngoma ya Tanasha inayojulikana kwa jina la Rider akiwa na msanii wa nchini Kenya, Kaligraph Jones.
Stori:HAPPYNESS MASUNGA, Ijumaa