Meneja: Kagere Ataendelea Kuwakera



MENEJA wa Meddie Kagere, Patrick Gakumba, amesema kama Kocha wa Simba, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck atampa nafasi mshambuliaji wake huyo basi ataendelea kuwakera wapinzani kwenye ligi ili atetee kiatu chake.


 


Kagere amefanikiwa kutwaa ufungaji bora misimu miwili mfululizo, 2018/19 alifunga mabao 23 na ule wa 2019/20 akitupia 22.




Hivi karibuni, Gakumba alitoa malalamiko juu ya mchezaji wake huyo kutokana na kutopata nafasi ya kucheza hali iliyosababisha Sven ampange kwenye mechi dhidi ya Biashara United ambapo alifanikiwa kutupia bao moja katika ushindi wa mabao 4-0 ambao Simba waliupata.


 


Akizungumza na Championi Jumamosi, Gakumba alisema anauamini uwezo wa Kagere kwa asilimia zote na iwapo atapewa nafasi zaidi kama ilivyo misimu iliyopita basi atatwaa kiatu cha dhahabu.


 


“Nashukuru uongozi wa Simba na mwalimu kwa nafasi aliyompa Kagere kwa kumuamini kwani ameleta furaha kwa Wanyarwanda ambao wamekuwa wakimfuatilia sana ndiyo maana APR ilikuwa ikimnyatia sana na walinifuata baada ya kuona hachezeshwi.


 


“Kagere ni mchezaji anayeelewa nini cha kufanya anapokuwa uwanjani, nimefurahi kuona amepata nafasi na amethibitisha kuwa bado ni yuleyule na ameonyesha uwezo, lakini naamini bado hajaonyesha kiwango chake, mechi za kimataifa ndio atakera sana.


 


“Iwapo ataendelea kupewa nafasi ndani ya kikosi cha Simba basi nina uhakika wa kuweza kutetea nafasi yake ya ufungaji bora kwani ni mchezaji mwenye kiwango kizuri hakuna asiyejua,” alisema Gakumba.


Kiswahili na Kifaransa hiyo ni kutokana na timu yao kuundwa na wachezaji wa mataifa mbalimbali wanaozungumza lugha hizo,” alisema mtoa taarifa huyo.


 


Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa timu hiyo, Frederick Mwakalebela kuzungumzia hilo alisema: “Hilo jukumu siyo letu ni la benchi la ufundi ambalo lipo chini ya kocha Zlatko, sisi tunahusika na masuala ya kiutawala pekee.”



Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad