Mgodi wa dhahabu wa DR Congo waporomoka na kuwaua watu 50



 Waokoaji wanachimba vifusi kufuatia kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu nchini DR Congo na kuwawacha watu takriban 50 wakiwa wamefariki.

Mgodi huo uliopo karibu na mji wa Kamituga , mashariki mwa taifa hilo uliporomoka siku ya ijumaa kufuatia mvua kubwa.


Maafisa wa eneo hilo wanasema kwamba wengi wa wale wanaohofiwa kufariki ni vijana wadogo na sasa wametoa wito wa siku mbili za maombolezi.


Ajali ni vitu vya kawaida katika sekta ta migodi nchini DR Congo ambayo ina viwnago duni vya usalama.


Mauzo ya dhahabu yapanda Uganda na kuzua mjadala


Kanda za video zilionesha watu wakijaribu kuchimba vifusi hivyo vilivyokuwa vinaziba mlango wa mgodi huo , huku waokoaji wakitumia vifaa wengine mikono yao kuondoa vifusi hivyo.


Gavana wa eneo hilo la mkoa wa kusini mwa Kivu , Theo Kasi alisema kwamba ameshutushwa na vifo hivyo vya watu 50 wengi wao wakiwa vijana.


Hatahivyo meya wa mji wa Kamituga, Alexandre Bundya alisema, hatuna hakika kuhusu idadi ya waliofariki, kilisema chombo cha habari cha AFP.


Shahidi mmoja aliambia AFP kwamba mvua kubwa ilisababisha maji kuingia katika mgodi huo, wakati watu walipojaribu kutoka, kulikuwa hakuna njia kwasababu maji yalikuwa yanaingia kwa wingi.


Bwana Kasi aliongezea kwamba ataidhinisha mikakati ya kuzuia ajali kama hizo kujirudia.


DR Congo ina hifadhi kubwa ya madini kama vile cobalt, almasi, shaba na dhahabu , lakini watu wake wanasalia kuwa miongoni mwa masikini zaidi duniani kutokana na miaka kadhaa ya vita na usimamizi mbaya.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad