Mgombea Ubunge Aahidi Kuanzisha Hifadhi ya Wanyamapori



Mgombea Ubunge Jimbo la Malinyi, kupitia NCCR-Mageuzi, Kennedy Chaya, amesema ikiwa wananchi watamchagua, atahakikisha inaanzishwa Hifadhi ya Wanyamapori ya Malinyi.


Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya kampeni, Chaya alisema katika wilaya ya Malinyi kuna mbuga kubwa na ndani yake kuna wanyama wa kila namna katika mbuga hiyo, ambayo kwa sasa serikali inaitambua kama pori tengefu.


Chaya alisema wilaya hiyo itakapokuwa na hifadhi kutakuwa na faida kubwa kwa kupata fedha za kigeni na kwamba mapato ya ndani yataongezeka na ajira zitakuwa nyingi kwa vijana.


Kuhusu elimu, alisema pamoja na serikali kutoa elimu bure kutoka shule za msingi hadi sekondari, ziko changamoto nyingi katika jimbo hilo ikiwamo uhaba wa walimu, vyumba vya madarasa na vifaa vya kufundishia hali ambayo inasababisha kushuka kwa kiwango cha ufaulu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad