Mgombea ubunge wa ccm aahidi kuwalipia wajasiriamali vitambulisho vya Magufuli



Mgombea ubunge jimbo la Tarime mjini kupitia Chama cha mainduzi (CCM),Nichael Kembaki ameahidi kuwalipia vitambulisho vya wajasilimali wafanyabiashara wadogo wadogo ili kuondokana na kamatwa kamatwa inayifanywa na  mgambo wa halmashauri.


Kembaki alisema jana katika mkutano wa kampeni mtaa wa Buguti kuwa akifanikiwa na kuwa mbunge atahakikisha anawalipia vitambulisho vya wajasiliamali na kuondokana na kamatwa kamatwa inayokuwa inaendeshwa na mgambo wa halmashauri.


"Ndugu zangu mkinichagua kuwa mbunge wenu nitahakikisha nawalipia vitambulisho vya wajasiliamali wafanyabiashara wadogo wa soko jipya la  Rebu ili kuondokana na adha ya kero ya kukamatwa na kufukuzwa katika maeneo mnayofanyia kazi"alisema Kembaki.


Mgombea huyo aliendambali zaidi na kusema kuwa kama akichaguliwa na kuwa mbunge ataenda kuunda Sacos kwa ajili ya wajasilia mali kwenda na kukopa fedha ya mtaji na wataende kurejesha mkopo huo taratibu na kwa malipo ya gharama nafuu kama sio kurudisha kiwango kilekile alichokopa mjasiliamali.


Kwa upande wa mgombea udiwani kata ya Turwa Chacha Musukuma aliwaomba wapiga kura kumchagua ili akajenge shule ya uwanja wa ndege/Buguti inayojengwa kwa nguvu za wananchi.


Nawaahidi ndugu zangu mkinichaguia na kuwa diwani wenu  nitahakikisha shule yetu inaenda kujengwa na wanafunzi kusoma karibu na kuwaondolewa kutembea mwando mrefu wa kufuata masomo shule ya msingi Rebu aliongeza kusema Musukuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad