WATU wanane, kati yao watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 25 mpaka 40, na watoto watano wanaokadiriwa kuwa na miaka miwili mpaka kumi, leo, Septemba 10, 2020, wamekutwa wakiwa wameuawa katika Hifadhi ya Isawima iliyopo wilayani Kaliua mkoani Tabora.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Barnabas Mwakalukwa, amethibitisha kukutwa kwa miili hiyo na kueleza kwamba uchunguzi wa kina unaendelea kubaini nini kilichosababisha vifo hivyo ambapo miili hiyo imekutwa ikiwa imeteketea kwa moto ndani ya hifadhi hiyo.
Amesema miili hiyo iligunduliwa na mfugaji aliyekuwa akitafuta mifugo yake hifadhini humo, ambapo baada ya kutoa taarifa, jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuongeza kwamba mpaka sasa bado chanzo cha vifo hivyo hakijajulikana